WATU WASIOJULIKANA WAMVAMIA NA KUMKATA MAPANGA DEREVA WA MBUNGE JOHN HECHE.

Dereva wa John Heche  Avamiwa na Kushambuliwa na Watu Wasiojulikana
Dereva wa Mbunge John Heche amevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga Mjini Tarime majira ya saa 2 usiku na hali yake siyo nzuri.

Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata