WAKAZI KAHAMA MJINI WALIA NA UKOSEFU WA NYAMA YA NG'OMBE KUFUATIA KUPANDA KWA BEI.Baadhi ya wakazi wa Mji wa KAHAMA mkoani SHINYANGA wameulalamikia uongozi wa wafanyabiashara wa nyama wilayani humo kwa kushindwa kutatua tatizo la ukosefu wa Nyama, linalochangia kupanda kwa bei ya nyama. 

Wakizungumza na Kijukuu Blog baadhi ya wakazi hao wamesema bucha nyingi zimefungwa na baadhi zenye Nyama huuza kilo moja kati ya shilingi  7,000 na 7,500, tofauti na awali  ambapo ilikuwa inauzwa shilingi 5,000 kwa kilo.

Mmoja wa wafanyabiasha wa nyama katika soko la nyahanga mjini Kahama, JACKSON MARO amesema kuwepo na changamoto ya upatikanaji wa nyama, kutokana na ng'ombe kupanda bei hali iliyochangia  bucha nyingi kufungwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa nyama Wilayani Kahama RENATUS ANDREA amesema nyama huenda iliadimika kipindi cha sikukuu ya Idd kwa sababu walichinja mifugo wachache ukilinganisha na mahitaji ya watu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama ABEL SHIJA amesema hadi sasa ofisi yake haijapata malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi na kwamba wanafuatilia suala hilo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata