VINGOZI WA NZENGO NYIHOGO KAHAMA,WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI WA MAPATO NA MATUMIZI.

SERIKALI ya mtaa wa Nyihogo  wilayani Kahama mkoani Shinyanga imewataka viongozi wa nzengo ya amani ‘B’ kutojishughulisha na shughuli zozote za nzengo hadi  uchunguzi  utakapofanyika kutokana na kukosekana kwa taarifa sahihi ya mapato na matumizi kuanzia 2013 hadi 2017.

Hatua hiyo imechukuliwa jana na mwenyekiti wa mtaa wa Nyihogo Daniel Mahela katika mkutano wa hadhara aliouitisha baada ya wananchi wa eneo hilo kumwandikia barua ya kumtaka aitishe mkutano huo kwa lengo la kutaka wasomewe mapato na matumizi.

Katika mkutano huo baada ya mwenyekiti huyo kusikiliza kilio cha wananchi hao kuwa hawana imani na viongozi wa nzengo hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake Solomon Juma kwamba taarifa ya mapato na matumizi ya kuanzia kipindi cha 2014-2017 haina uwiano sawa na idadi ya ongezeko la watu wanaohamia katika eneo hilo hali ambayo Mahela aliwataka viongozi hao wapishe uchunguzi.

Pia Mahela ameeleza kuwa kutokana na wananchi wa nzengo hiyo kufanya mikutano ya mara kwa mara kwaajili ya kusomewa taarifa ya mapato na matumizi huku vikao vyao vikiwa vinaishia njiani kwa kuhofia uvunjifu wa amani hivyo walichukua uamuzi wa kutaka ofisi ya mtaa isimamie zoezi hilo jambo ambalo ametekeleza.

Kwa upande wao wananchi wa nzengo hiyo walidai kuwa walichukua uamuzi huo kutokana na nzengo hiyo idadi ya watu kuzidi kuongezeka jambo ambalo linasababisha vyombo kupungua msibani na watu kusubiliana wakati wa chakula hali ambayo wamehofia kukuambukizana maradhi yatokanayo na kinywa.

Naye mhasibu upande wa wanawake Yunis Masalu akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya nzengo kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 alisema kuwa jumla ya mapato yote ni shilingi ya viingilio katika nzengo ni 519,000 matumizi ni shilingi 141,000  na fedha iliyopo hadi sasa ni shilingi 319,00.

Kwa upande wake mwenyekiti wa nzengo hiyo Solomoni Juma alisema atamfungulia mashataka mwenyekiti kwa kitendo cha kumdhalilisha kuwa wamefuja mali za nzengo.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata