TAHARUKI KAHAMA:FISI AKUTWA NDANI YA HOSPITALI YA WILAYA MJINI KAHAMA.Katika hali isiyokuwa ya kawaida wagonjwa na watu waliokuwa katika hospitali ya Mji wa Kahama wameingia katika hali ya taharuki na kuanza kushangaa baada ya Fisi mmoja kuonekana kirandaranda ndani ya eneo la hospitali hiyo leo asubuhi.

Akizungumza na Kijukuu Blog ofisini kwake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dr. LUCAS DAVID amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 12 alfajiri ambapo Fisi huyo ambaye mpaka sasa haijulikani alitokea wapi, alipoingia ndani ya hospitali hiyo.

Amesema kuwa licha ya eneo la Hospitali hiyo kuwa na uzio  mkubwa fisi huyo aliingilia katika chuo cha Manesi ambapo kuna tundu la linalopitia karibu na chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi  wa Hospitali hiyo, Dkt. FREDIRICK MALUNDE amesema kuwa baada ya kuonekana walimuarifu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji ambaye aliwaarifu watu wa Idara ya Maliasili ambao walifanikiwa kumuua fisi huyo kwa kumpiga risasi tatu.

TUKIO la fisi huyo linakuja siku moja baada ya taarifa kuwa kundi la Fisi limevamia na kukatakata mabomba ya maji ya Mradi wa Kilimo cha Mbogamboga wa Kikundi cha Songambele katika kata ya Nyandekwa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata