SAKATA LA UMILIKI WA MAENEO YA VIWANJA KAHAMA ENEO LA TRA....NAIBU WAZIRI WA ARDHI ASEMA NI ENEO LA HALMASHAURI ALIYEONA KAZULUMIWA AENDE MAHAKAMANI.Serikali imesema eneo la mlima wa TRA-MALUNGA ambalo lina mgogoro kati ya halmashauri ya mji wa KAHAMA na baadhi ya Wakazi ni mali halali ya halmashauri hiyo.

Akizungumza jana katika ziara yake ya kikazi wilayani KAHAMA, Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ANGELINA MABULA amesema amejiridhisha na ufuatiliaji uliofanywa na ngazi zote husika za serikali.

Amesema kuanzia sasa mlima huo ni mali halali ya halmashauri ya mji wa KAHAMA kwa ajili ya ujenzi wa taasisi za umma kama ofisi sambamba na uwekezaji mwingine wa serikali.

Hata hivyo MABULA amewataka wakazi hao kwenda mahakamani wakiwa na vielelezo vyote vya umiliki wa maeneo hayo endapo hawakuridhika na maamuzi yaliyotolewa na serikali.

Mapema, baadhi ya wakazi wanaodai kuwa wamiliki wa maeneo hayo wamemwambia Naibu Waziri MABULA kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo kwa sababu baadhi yao wamepewa vibali vya umiliki na halmashauri hiyo ya Mji wa Kahama.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata