ROONEY AKAMATWA NA POLISI AKIWA ANAENDESHA GARI HUKU AMELEWA


Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney amekamatwa na baadae kuachiliwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa, polisi mjini Cheshire imesema.

Rooney alikamatwa baada ya polisi kusimamisha gari aina ya Volkswagen Beetle ambayo alikuwa anaendesha. Polisi wa Cheshire wanasema Rooney mwenye miaka 31, ana mashtaka ya kujibu kwa kukutwa akiendesha gari akiwa amelewa na akiwa pia kwenye mwendo mkali.

Nahodha huyo wa zamani wa England na Manchester United ameachiliwa, lakini kesi yake itasikilizwa baadae mwezi huu. Rooney ambaye amestaafu soka la kimataifa mwezi uliopita, ndiye anashikilia rekodi ya ufungaji mabao muda wote kwenye timu ya taifa akiwa na magoli 53.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata