NATAMANI KUONGEA HALI YA USALAMA NCHINI NA MASHAMBULIO ILA NAHOFIA USALAMA WANGU- NEY WA MITEGO

Natamani Kuongea Hali ya Usalama Nchini na Mashambulio ila Nahofia Usalama Wangu- Ney wa Mitego
Msanii Ney Wamitego kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu hali ya usalama ilivyo hapa nchini kufuatia matukio ya mauaji ya watu mbali mbali, na shambulio la risasi la Tundu Lissu ambalo limetikisa nchi nzima.

 Ney amesema ingawa wasanii ndiyo watu ambao wakipaza sauti zao zinaeleweka kwa wengi hata wasiofuatilia siasa, lakini ameona bora ayaache masuala hayo kwa wenyewe wanasiasa kutokana na uoga alionao.
Ney ameendelea kwa kusema kwamba anatamani kuongea lakini kutokana na hali ilivyo kwa sasa anahofia usalama wake, maana mpaka familia yake inamkalisha chini kumuonya na kuamua kukaa kimya, na kuwaachia wanasiasa waendelee kupambana wenyewe

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata