MAAJABU KAHAMA,FISI WATAFUNA BOMBA LA MAJI NA KUSABABISHA HUDUMA KUKOSEKANA.Katika hali isiyokuwa ya kawaida wanyama wanaosadikiwa kuwa Fisi wametafuna mabomba ya maji na kuharibu mtandao huo katika kata ya Nyandekwa halmashauri ya mji wa Kahama.

Akizungumza leo na Kijukuu blog Diwani wa kata ya Nyandekwa KULWA KADEBE amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ikiwa ni siku moja baada ya fisi kudaiwa kula kuku  40 katika kijiji cha Kakebe.

KADEBE amesema fisi hao wameshambulia kwa meno na kuyatoboa mabomba hayo  katika chanzo cha maji na kusababisha maji kushindwa kufika kwenye eneo la Mradi wa umwagiliaji wa mboga na matunda wa kikundi cha songambele ulipo Nyandekwa.

Kutokana na hali hiyo      KADEBE amesema tayari ametoa taarifa kwa serikali ambapo mkurugenzi wa halmashauri ameahidi kupeleka maafisa wa wanyamapori  kwa ajili ya kusaidia kuwawinda wanyama hao.

Juzi fisi mmoja aliuwawa na wanachi katika kijiji cha Kakebe baada ya kukutwa ndani ya banda la kuku la mkazi wa kijiji hicho  akiwa tayari amekula kuku 40.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata