KIWANDA CHA NYAYA ZA UMEME CHAWAKA MOTO LEO

Kiwanda cha nyaya za umeme chawaka moto leo
Kiwanda chote cha  Multi Cable Limited kilichopo  eneo la Kijereshi kata ya Igoma jijini Mwanza ,kimeteketea kwa  moto leo.

Kiwanda hicho kimeanza kuwaka saa nne mchana kutokana hukuchanzo kikibainika ni  hitilafu ya nguvu za umeme.

Kiwanda hicho cha Multi Cable Limited kinajihusisha na utengenezaji wa nyaya za umeme na bomba za kupitisha nyaya hizo.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda hicho, anasema wao walishtukia moshi ukiwa unatokea  kwenye 'store'  wakagundua kwamba ni nyaya zimegusana kwenye paa na kusababisha moto huo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata