JWTZ LAWARUDIA WANANCHI


Jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, limewaomba Watanzania wote waliunge mkono Jeshi hilo na kwamba, liko imara na tayari kuilinda Nchi, kuilinda na na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa uaminifu Serikali .
Akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam leo, kuhusu miaka 53 tangu kuasisiwa kwake, Mkuu wa Majeshi Nchini, Jenerali Venance Mabeyo, amesema, wakati JWTZ inaandika historia ndefu imefikia mafanikio mbalimbali, ikiwemo kudumisha amani na utulivu uliopo nchini tangu Uhuru, limeshiriki Vita vya ukombozi Kusini mwa Afrika, Vita vya Kagera na Visiwa vya Comoros.
Jenerali Mabeyo amesema, JWTZ pia limekuwa ni nguzo muhimu katika kudumisha amani sehemu mbalimbali duniani kwa kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani, katika nchi za Liberia, DRC, Sudan , Lebanon, Sudan Kusini, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Aidha, amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli, Baraza la Mawaziri,pamoja na Viongozi Wakuu wa Serikali kwa Maelekezo mbalimbali wanayoyatoa kwa Jeshi ushauri ambao umekuwa muhimili mkubwa kwa utendaji wake.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata