JOSHUA NASSARI AMJIBU POLEPOLE

Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari amefunguka kwa kumjibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole kwamba amemsikia alichokizungumza na kuahidi akirudi Tanzania ataweka ukweli wote hadharani.

Nassari amebainisha kupitia ukurasa wake maalum wa facebook jioni ya leo baada ya kusikia kauli kutoka kwa Humphrey Polepole ikidai kama kweli viongozi wa upinzani wanaushahidi wa rushwa ama kununuliwa madiwani waliohamia CCM wakitokea CHADEMA basi wanapaswa kuweka hadharani kwa kutaja hata majina ya wahusika na sio kulingishia.

"Nimemsikia ndugu Polepole. Nipo Nairobi, nikirejea tu nyumbani Tanzania nitaweka hadharani ushahidi huu, usiokuwa hata na chembe moja ya shaka. Ili tuone kama kweli CCM itachukua hatua kwa wateule wa rais", ameandika Nassari.

Hayo yote yamekuja baada ya kupita takribani siku mbili tokea mbunge Joshua Nassari kudai ana ushahidi usiotia shaka juu ya madiwani ambao wamepokelewa na Rais Magufuli wakati alipokuwa katika ziara yake mkoani Arusha kuwa wamenunuliwa na kupewa rushwa na siyo kwamba wamehama kwa lengo la kukubali kazi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata