JESHI LA ZIMAMOTO MWANZA LAWATADHALISHA MAMA LISHE KUCHUKUA TAHADHARI ZA MOTO.

Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Mwanza limewatahadhalisha mama lishe pamoja na wafanyabiashara wengine kukumbuka kuzima moto baada ya kumaliza shughuli zao za biashara ili kuepuka majanga ya moto kuteketeza masoko na kusababisha watu kupoteza maisha na mali zao.

Tahadhari hiyo inatolewa na kamishna msaidizi wa jeshi hilo mkoani Mwanza Andrew Mbate wakati akitoa elimu ya kujikinga na majanga ya moto kwa wafanyabiashara wa ndani wa soko kuu la Mwanza pamoja na kuzindua namba mpya ya huduma ambayo ni 114 itakayokuwa ikitumiwa na wananchi kwa ajili ya kutoa taarifa pindi majanga ya moto yatokeapo.

Changamoto kubwa katika kujihami na majanga ya moto ndani ya soko hilo lenye zaidi ya wafanyabiashara 700 ni uwepo wa milango midogomidogo 7 na mlango mkubwa mmoja, ambayo wafanyabiashara hawa wanasema haiwezi kuhimili mikikimiki pindi majanga ya moto yatokeapo.

Hamad Nchola ni mwenyekiti wa soko kuu Mwanza, anaiomba halmashauri ya jiji la Mwanza inayosimamia soko hilo kuongeza ukubwa wa milango iliyopo hivi sasa ili kukabiliana na hali ya majanga ya moto yanayoweza kujitokeza.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata