HALMASHAURI YA USHETU IMEKANUSHA TAARIFA ZA UKOSEFU WA MAJI KATIKA KATA YA UKUNEHalmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, imekanusha taarifa za kuwepo kwa changamoto ya maji katika kata ya Ukune,  inayosababishwa na kukosekana kwa mafuta ya kuendesha mtambo wa kuvuta maji hayo.

Akizungumza na Kijukuu Blog leo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo MICHAEL MATOMOLA amesema halmashauri yake imetoa zaidi ya shilingi milioni 1 za ununuzi wa mafuta, huku shule ya sekondari Dakama nao wakitoa shilingi laki 4.

MATOMOLA ameongeza kuwa utafiti uliofanywa kwa mkoa wa SHINYANGA wiki iliyopita, mradi wa maji wa Kayenze ambao ndio unaohudumia kata ya Ukune, umeshika nafasi ya pili ukitanguliwa na BULUNGWA.

Kuhusu mchango wa Shilingi 14,000/= kila kaya ili kupata maji, na bei ya shilingi 50 kila ndoo ya maji, MATOMOLA amesema hilo hawezi kulizungumzia kwasababu ni makubaliano baina ya wananchi na viongozi wa kijiji husika. 

Hivi karibuni baadhi wananchi wa kata ya Ukune walilalamikia kukatika kwa maji kila mara  bila taarifa hali iliyokuwa ikiwapa wakati mgumu wa  kupata maji, na kujikuta wanatumia maji yasiyo salama kwa afya.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata