DR CONGO: KIONGOZI WA UPINZANI AREJEA MJINI KINSHASA

Kiongozi wa muungano wa upinzani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo arejea mjini Kinshasa

Felix Tshisekedi, kiongozi wa muungano wa upinzani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  amerejea mjini Kinshasa katika kipindi ambacho watu wamekamatwa.

Hali tete imejitokeza mjini Kinshasa baada ya kupigwa marufuku  mkutano  wa upinzani .

Felix Tshisekedi aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa  wa Ndjili Jumapili huku akisubiriwa na wafuasia wake.

Polisi mjini Kinshasa  iliwazuia wafuasi wa upinzani  kusogelea uwanja wa ndege kumpokea Felix Tshisekedi.

Tshisekedi alipokelewa na jeshi la Polisi lililomlindia usalama.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata