CWT KAHAMA WALIA NA UPUNGUFU WA WALIMU NA IDADI KUBWA YA WANAFUNZI.

Uhaba wa walimu na idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za msingi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, imeelezwa kuwa sababu inayochangia wanafunzi kutopata elimu ipasavyo.

Hayo yamebainishwa leo na Katibu wa Chama cha Walimu  (CWT) Wilaya ya Kahama Mwalimu DAUDA MOHAMMAD BILIKESI wakati akizungumza na Kijukuu Blog ofisini kwake kuhusiana na Uhaba wa Walimu katika Shule za Msingi.

Amesema tangu serikali ilipoanza kutekeleza zoezi la kukagua vyeti batili katika sekta mbalimbali, Walimu wengi wamefukuzwa kazi na kwamba mpaka sasa  serikali haijaajiri walimu  wengine ili kuziba pengo la walioondoka.

Akizungumzia madai ya walimu, BILIKESI amesema Serikali  inatarajia kulipa Madeni ya Walimu  wakati wowote  na kuwataka  kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu katika vituo vyao vya kazi.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata