BODA BODA KAHAMA WATAKIWA KUKATA LESENI ZA USAFIRISHAJI HARAKA IWEZEKANAVYO.Waandesha bodaboda wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujisajili na kukukata  leseni ya usafirishaji ili kuepuka hatua za kisheria dhidi yao ikiwemo kutozwa faini.

Akizungumza na waendesha bodaboda katika kituo cha Namanga mjini Kahama leo, Afisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini na Majini (SUMATRA) mkoani Shinyanga JOSEPH MASWE amesema zoezi hilo limekwisha kamilika katika Halmashauri nyingine za wilaya ya Kahama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Kahama, ROBERT SEWANDO amesema kuanzia muda huu vituo vyote vya bodaboda katika Halmashauri ya mji Kahama havitatambulika rasmi mpaka watakaposajili leseni hizo za usafirishaji.

Wakizungumzia zoezi hilo baadhi ya Waendesha bodaboda wamesema kuwa Wameliopokea agizo hilo lakini wameomba waongozewe muda ili waweze kujisaji pamoja na kukata leseni hizo za usafirishaji.

Halmashauri ya Mji wa Kahama unakadiriwa kuwa na bodaboda zaidi 6,000 huku nyingi zikiwa hazijasajiliwa rasmi, hali inayotoa mwanya kwa baadhi ya Wahalifu wakiwemo Wahamiaji haramu kujificha kwenye mgongo wa biashara hiyo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata