SERIKALI WILAYANI KAHAMA YAPIGA MARUFUKU UCHIMBAJI WA MADINI ENEO LA SHUNU NYAHANGA.



 KAHAMA
SERIKALI wilayani Kahama mkoani Shinyanga imepiga marufuku uchimbaji wa madini katika eneo la Shunu kata ya Nyahanga wilayani humo kufuatia kuibuka kwa tetesi jana kuwa eneo hilo lina madini ya dhahabu.

Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhil Nkulu wakati akiongea na Kahama Fm kuhusu hatua waliofikia kufuatia wananchi kuingia katika eneo hilo na kuanza kuchimba dhahabu pasipo kuwa na kibali.

Nkulu amesema kuwa hakuna ruhusa kwa  mtu yeyote kuchimba dhahabu katika eneo hilo na ameliagiza jeshi la Polisi kumkamata yeyote atakayepatikana anafanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.

Sambamba na hayo Nkulu ameongeza kuwa uchimbaji wa madini una sheria zake hivyo kama mtu anataka kuchimba akate kibali katika ofisi za madini na afuate taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwahamisha wakazi wa maeneo hayo na kuwalipa fidia.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyahanga Maiko Magile amesema kuwa siku ya leo watu siyo wengi kama ilivyokuwa jana na kwamba wanaanza kupungua kutokana na kukosa dhahabu.

Magile ameongeza kuwa kwa sasa kuna uharibifu na uchafuzi mkubwa wa mazingira uliosababishwa na uchimbaji wa Mashimo sambamba na watu kujisaidia ovyo katika eneo hilo kutokana na kutokuwa na vyoo.

 MATUKIO KATIKA PICHA:


WANANCHI WAKIWA KATIKA ENEO AMBALO LINASADIKIWA KUWA NA DHAHABU.

WANANCHI WAKICHUNGULIA SHIMO AMBALO INASEMAKANA NDILO LENYE DHAHABU.


WANANCHI WAKIENDELEA KUCHIMBA MCHANGA KATIKA ENEO LA SHUNU MJINI KAHAMA.
KINA MAMA,VIJANA,WAZEE NA WATOTO WAKIZOA MCHANGA NA KUCHIMBA UDONGO KATIKA ENEO HILO.

MZEE AMBAYE HAKUFAHAMIKA JINA LAKE AKIWA NA VIFURUSHI VYA MCHANGA BAADA YA KUCHIMBA KATIKA ENEO HILO.
WANANCHI WAKIZIDI KUMIMINIKA KUJITAFUTIA RIDHIKI KATIKA ENEO HILO.

AFISA WA JESHI LA POLISI AKIWAZUIA WANANCHI KUINGIA KATIKA ENEO HILO JANA.


WANANCHI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA WA JESHI LA POLISI KUHUSU KUTOINGIA KATIKA ENEO HILO



SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata