WALIMU WASTAAFU WAGAWIWA MABATI KAHAMA,CWT MKOA YAWAASA KUHUSU KIINUA MGONGO.

 WALIMU WASTAAFU WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU CWT MKOA NA WILAYA.


KAHAMA
Chama cha walimu mkoa wa Shinyanga CWT kimewaasa walimu wastaafu wilayani Kahama mkoani Shinyanga kutumia vizuri Kiunua mgongo wanachopata baada ya kustaafu na kuacha tabaia ya matumizi mabaya ya fedha katika Starehe.

Wito huo umetolewa leo mjini Kahama na mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Shinyanga George Nyangusu,wakati akiwakabidhi mabati 20 kila mmoja walimu kumi waliostaafu mwaka huu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Nyangusu amesema kumekuwa na baadhi ya walimu wenye tabia ya kutumia vibaya fedha za kiinua mgongo vibaya kwa kuzifanya kuwa viinua migongo kwa kufanya starehe na watu wengi pamoja na  kupoteza pesa kwa kutapeliwa katika biashara zisizo halali.

Naye mwenyekiti wa Chama hicho Wilayani Kahama Victor Tandise amesema kuwa ukomo wa kuwa mtumishi wa umma kupitia sekta ya elimu siyo sababu ya kujutia kwani kuna kazi zingi za kufanya katika jamii zikiwemo ujasiliamali,ufugaji na kilimo.

Awali akitoa utambulisho katibu wa chama cha walimu wilaya ya Kahama Dauda Billcase amesema kuwa chama cha walimu kina desturi ya kutoa mabati ishirini yenye urefu futi kumi na Gage 30 ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao katika Chama.

Akiwataja walimu waliopatiwa mabati hayo Billcase amewataja kuwa ni Mkono Lufunga,Malangaye Sengerema,Wanga Mathew,Cristina Benjamini,Charlles Kalabo,Tekla Boniface,Andrew Mayombo,Grace Oswald na Simon Malombo.

Akiongea kwa niaba ya Walimu wanaostaafu mwalimu  Simon Mbagale aliyestaafu kotoka shule ya Malunga ameshukuru kwa msaada huo wa mabati waliyopatiwa na kutoa rai kwa walimu waliopo kazini kuzingatia maadili ya kazi muda wote watakapokuwa kwenye utumishi.

MATUKIO KATIKA PICHA: 
 
 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA SHINYANGA GEORGE NYANGUSU AKIZUNGUMZA NA WALIMU WASTAAFU KATIKA GHAFLA HIYO.


 WALIMU WASTAAFU WAKIWA NA BAADHI YA NDUGU ZAO WALIPOFIKA KATIKA OFISI ZA CHAMA CHA WALIMU CWT KAHAMA KUPOKEA MABATI YAO.

 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA VICTOR TANDISE AKITOA NENO KWA WALIMU WASTAAFU KATIKA GHAFLA HIYO.

 WALIMU WASTAAFU WAKISIKILIZA KWA MAKINI WOSIA WA MWENYEKITI WA CWT MKOA HAYUPO PICHANI.

 WALIMU WASTAAFU WAKIENDELEA KUPOKEA WOSIA KUTOKA KWA VIONGOZI WA CWT KATIKA GHAFLA YA KUKABIDHIWA MABATI.

 WALIMU WASTAAFU WAKIENDELEA KUPOKEA MAWAIDHA KUTOKA KWA VIONGOZI WA CWT.

 MWALIMU MSTAAFU GRACE OSWALD KUTOKA SHULE YA MSINGI KILIMA "B" AKISIKILIZA KWA MAKINI WOSIA WA MWENYEKITI WA CWT MKOA WA SHINYANGA,HUYU NDIYE ALIYEKUWA MWALIMU BORA WA HESABU KWA WILAYA YA KAHAMA KATIKA MIAKA YAKE AKIWA KAZINI.

 MWALIMU SIMONI MBAGALE,MWALIMU MSTAAFU KUTOKA SHULE YA MSINGI MALUNGA AKISIKILIZA KWA MAKINI USHAURI WA VIONGOZI WA CWT...PEMBENI KUSHOTO NI MJOMBA WAKE ALIYEMSINDIKIZA KATIKA GHAFLA HIYO.

 GHAFLA IKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA OFISI ZA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA.

 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA SHINYANGA GEORGE NYANGUSU AKIMKABIDHI RISITI YA MABATI MWALIMU SIMONI MBAGALE ALIYESTAAFU KUTOKA SHULE YA MSINGI MALUNGA.

 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA SHINYANGA GEORGE NYANGUSU AKIMKABIDHI RISITI YA MABATI MWALIMU MSTAAFU TEKLA BONIFACE KUTOKA SHULE YA MSINGI KILIMA "B". WALIMU WASTAAFU WAKIWA NA UONGOZI WA CWT MKOA NA WILAYA WAKIWA NA ZAWDI YA MABATI YAO.

 MWEKA HAZINA WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA HARUNA KAMBI AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI UBORA WA MABATI WANAYOWAGAWIA WALIMU WASTAAFU.

 MWALIMU MSTAAFU SIMON MBAGALE BAADA YA KUMKABIDHI MKE WAKE RISITI YA MABATI HUKU AKISEMA KUWA BILA MKEWE ASINGEFIKA HAPO.

 BAADA YA SHUGHULI YA KUKABIDHI MABATI WALIMU WASTAAFU WALIPATA NAFASI YA KUPATA CHAKULA CHA PAMOJA.

 WALIMU WAKIENDELEA KUCHUKUA CHAKULA

 WALIMU WASTAAFU NA VIONGOZI WAKIFURAHIA CHAKULA KIZURI TOKA KAMPUNI YA MUBASHARA FOOD SERVICES

 KITU CHA MAHARAGE HICHO

 KATIBU WA CWT KAHAMA AKICHUKUA CHAKULA BAADA YA SHUGHULI ZA MAKABIDHIANO YA MABATI.

 WAGENI WAALIKWA WAKIPAKUA CHAKULA 


                PICHA ZOTE NA WILLIAM BUNDALA (KIJUKUU CHA BIBI K)

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata