UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA, WANANCHI WA WILAYA YA RORYA WANAHANGAIKAZaidi ya wananchi elfu mbili wanaoishi katika vijiji vitatu vya Rwang’enyi, Busanga na makongeni vilivyopo katika kata ya Nyamtinga wilayani Rorya mkoani Mara wanakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama hali inayowalazimu kuamka usiku wa manane kwenda kwenye mwambao wa ziwa victoria kwa ajili ya kufuata huduma ya maji.

Wakizungumza katika mkutano uliowakutanisha na naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo wananchi hao wamesema wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu huku wakati mwengine wakiamka usiku wa manane kwaajili ya kufuata huduma ya maji katika ziwa Victoria.

Kero ya wananchi hao inamfikia naibu waziri Jaffo na hapa anatoa agizo ambalo linalotoa taswira njema ya kutatua tatizo lao.

Katika hatua nyingine naibu waziri JAFFO akapata fursa ya kuzungumza na watumishi wa halmashauri ya rorya na kuwataka watumishi wote kufanya kazi kwa kuzingatia weledi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata