TFF WATOA NGAO MPYA KWA SIMBA

HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefanya marekebisho katika Ngao ya Jamii ambayo timu ya Simba ilikabidhiwa baada ya kuifunga Yanga, Jumatano iliyopita.

Awali Ngao hiyo ilikosewa katika neno SHIELD, Simba walikabidhiwa lakini baada ya makosa kuonekana, TFF waliomba radhi kesho yake kisha kuwaambia Simba wairejeshe Ngao hiyo kwa ajili ya marekebisho ya neno hilo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas ameionyesha Ngao iliyorekebishwa kwa waandishi wa habari leo Jumanne kwenye ofisi za shirikisho hilo, Karume jijini Dar.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata