TFF KUWAADHIBU WALIOKOSEA KUANDIKA SPELLING KWENYE NGAO YA HISANI.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23.

TFF imesema Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hawajapokea vizuri mwonekana wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

-Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi" Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Na kuongeza kuwa "Hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena,".

Simba Bingwa. 
Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliowakutanisha timu za Simba SC na Yanga SC za Dar es Salaam kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa Jijini humo.

Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo baada ya dakika 20 kumalizika kwa Suluhu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata