TAHADHARI YATOLEWA KUTOKANA NA JOTO KALI ULAYA

Baadhi ya maeneo barani Ulaya yanashuhudia viwango vya juu zaidi vya joto katika kipindi cha mwongo mmoja, baadhi ya maeneo vikipokea hadi nyuzi joto 44C (111 F).

Mataifa kadha yametoa tahadhari kwa wakazi wiki hii, Joto kali nchini Italia limesababisha moto porini na miji kadha imewekwa katika hali ya tahadhari.

Wimbi la joto limesababisha baadhi ya maeneo kukabiliwa na hatari ya ukame mbaya.

43C mjini Roma.
Tahadhari ya kiafya imetolewa katika baadhi ya maeneo ambayo viwango vya joto vimepanda kiasi cha kuwa hatari kwa maisha.

Italia inashuhudia viwango vya joto ambavyo ni nyuzi joto 10C juu ya kiwango cha wastani kipindi sawa na cha sasa cha mwaka.

Wananchi wameshauriwa kusalia manyumbani na kunywa maji kwa wingi, Jumatano, viwango vya joto vilifikia 44C eneo la Sardinia.

Alhamisi, joto lilifikia nyuzi joto 43C karibu na jiji la Roma nako Sicily viwango vya joto vikafikia nyuzi joto 42C huku wingu la hewa yenye joto kali likivuma kutoka Afrika kupitia bahari ya Mediterranean.

Watalii na wenyeji wamekuwa wakipoesha joto kusini mwa Afrika kwa kutumia maji kwenye chemchemi za miji.

Hali ya sasa inatarajiwa kuendelea hadi Jumatatu. Hali ya tahadhari imetolewa katika miji 26 Ulaya.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata