SEARCH FOR COMMON GROUND WATOA ELIMU KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI MSALALA KWA LENGO LA KUJIFUNZA KUTATUA MIGOGORO KATIKA JAMII INAYOWAZUNGUKA.MRATIBU WA MAFUNZO WA SHIRIKA LA SFCG DAVID NTIRUKA AKIELEZEA NAMNA SHIRIKA LINAVYOANYA KAZI NA JESHI LA POLISI.

KAHAMA
Jamii Katika Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga imetakiwa kuwashirikisha vijana hususani wanafunzi katika utatuzi wa migogoro katika jamii ili kudumisha amani katika Maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Program Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Seach for Common Ground, kwenye halfa ya kuzindua mradi wa kuwajengea uwezo Wanafunzi 80 kutoka Katika Halmashauri hiyo.

Amesema endapo jamii itaona umuhimu wa kuwashirikisha vijana katika utatuzi wa migogoro inayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwenye maeneo yao, maendeleo yapatika kwa haraka.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mradi huo, DAVID NTIRUKA amesema mradi huo utawafikia wanafunzi 80 kutoka shule za sekondari za Bugarama na Bulyankulu zilizopo katika Halmashauri ya Msalala.

Naye afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Msalala MERRY KISAMAKA amesema serikali inaendelea kuhamasisha kuanzishwa kwa Klabu za kupambana na Rushwa katika shule za msingi na sekondari ili ziweze kuwasaidia kukabilana na migogoro.

Hafla ya uzinduzi huo ulioambatana na mafunzo kwa wananfunzi ambayo imenza leo itafanyika kwa  siku mbili mjini Kahama kwa Udhamini wa Shirika lisilo la kiserikali la Seach for Common Ground.
 

  
 
BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE ZA BUGARAMA NA BULYANHULU WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI PROGRAM MANAGER WA SHIRIKA LA SFCG HAYUPO PICHANI.

 
WANAFUNZI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA NAMNA SHIRIKA LA SFCG LINAVYOFANYA KAZI NA HALMASHAURI YA MSALALA.

 
BAADHI YA WALIMU WALIOAMBATANA NA WANAFUNZI WAKISIKILIZA KWA MAKINI
WANAFUNZI WAKITAZAMA KWA MAKINI NAMNA SHIRIKA LA SFCG LINAVYOFANYA KAZI NA JAMII KATIKA KUTATUA/KUSULUHISHA MIGOGORO
 
WANAFUNZI WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAELEKEZO YA WAWEZESHAJI AMBAO NI SFCG.PICHA NA SALVATORY KELVIN


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata