RUSHWA YATAJWA KUWA CHANZO CHA UGUMU WA KUMLINDA MTOTO KATIKA MAENEO MENGI.Baadhi ya wadau wa haki na  ulinzi wa Mtoto  wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamesema jitihada za kumlinda mtoto zinakwama kutokana na maeneo mengi yanayotoa haki kugubikwa na vitendo vya Rushwa. 

Hayo yameelezwa leo na wachangia mada mbalimbali katika kikao cha kutambulisha mradi wa HAKI NA ULINZI WA MTOTO unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la RAFIKI-SDO kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la SAVE THE CHILDREN.

Akichangia mada hiyo ya namna bora ya  kumlinda mtoto, Diwani wa kata ya Kagongwa HAMIS KASHANTOLE  amesema tatizo kubwa ni watu waliopewa dhamana ya kutoa haki  kuendelea kuwakandamiza watoto.

Amesema ipo haja ya kuona namna bora ya kutoa elimu kwa watoa maamuzi kama mahakama ili wapunguze mlolongo wa kutoa haki kwa watoto jambo litakalosaidia watoto kupata haki zao.

Kwa upande wao baadhi ya watoto waliokuwepo kwenye kikao hicho  wamesema watoto wengi wamekuwa wakibakwa, kunyanyaswa na watu au wazazi lakini bado haki zao  zimekuwa hazipatiwi nafasi katika kuzijadili.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika zoezi la kutambulisha mradi huo, Diwani wa kahama mjini HAMIDU JUMA  amesema ikiwa elimu itatolewa ipasavyo katika  ulinzi  wa mtoto, haki zao zitapatikana.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata