MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AVUTIWA NA NYIMBO MPYA YA ALI KIBA ‘SEDUCE ME’

Baada ya mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ August 25, 2017, wimbo huo umeonekana kupokelewa vizuri hata na viongozi wa kisiasa ambao hawakuficha hisia zao.

Mmoja wa wanasiasa ambao wameonesha kuupokea vizuri wimbo huo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ambaye alitumia Instagram yake kuuelezea.

DC Hapi aliandika”Nimekuelewa sanaa wajina @officialalikiba. Kazi imeenda shule. Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli. Keep the fire burning!🔥 #seduceme.”

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata