MKE WA MUGABE AMPA VITASA BINTI

Rais Robert Mugabe na mkewe, Grace Mugabe.

Mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe anatuhumiwa kumpiga na kumsabababishia majeraha binti mmoja aliyemkuta na wanawe wawili wa kiume mjini Johannesburg, Afrika Kusini jana Agosti 13 alikokuwa amekwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya mguu.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Bulawayo 24 ya nchini Zimbabwe na jumbe mbalimbali zilizotumwa kupitia mtandao wa Twitter mjini Johannesburg na Harare, zimedai kuwa Grace Mugabe alimshambulia binti aliyefahamika kwa jina la Gaby kwa kutumia waya wa umeme baada ya kumkuta na wanae wawili, Robert Jr (25) na Chatunga (21).
Gaby aliyejeruhiwa.
 
Watoto hao wawili ambao wapo mjini humo kimasomo wanafahamika kwa kula bata zaidi kuliko kusoma, kitu ambacho ndio lengo la wao kuwepo nchini humo.

Hivi karibuni Robert Mugabe Jr, na Chatunga Bellarmine,  walifukuzwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi eneo la Rivonia baada ya kusababisha usumbufu kutokana na kelele za muziki na watu waliokuwa wakija katika nyumba hiyo. Hata baada ya kufukuzwa, walitakiwa kuikarabati nyumba hiyo.

Msichana huyo aliyepigwa na Grace alipata jeraha kichwani kwake na kwamba walinzi walikuwa wakishuhudia namna anavyoshambuliwa na mke huyo wa Rais wa Zimbabwe.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata