MASTAA WALIOHUDHURIA PAMBANO LA FLOYD MAYWEATHER V MCGR

 Jiji la La Vegas wiki hii lilikuwa busy sana kusubiri kwa hamu pambano lililopigwa asubuhi ya leo kati ya mbabe wa boxing Floyd Mayweather na Conor McGregor mbabe wa UFC.

Gregor alifanikiwa kwenda hadi raundi ya 3 akiongoza na baadae kuanzia raundi ya 4 kuonekana kuchoka sana kitu kilichompelekea kushambuliwa hadi raundi ya 10 kumalizwa kabisa kwa TKO.

Mchezo huu ambao baadhi ya siti za uwanja zilikuwa tupu ulihudhuriwa na masupastaa wengi kutoka nchini Marekani akiwemo mbabe wa zamani wa ndondi Mike Tyson.


 Mwanamuziki wa Hip Hop Sean Combs almaarufu kama P Diddy naye alikuwepi uwanjani hapo kumpa sapoti Mayweather ambaye ni mshkaji wake.

 Leaornardo Di Caprio mshindi wa tuzo ya Oscar alihudhuria pia katika mchezo wa leo asubuhi.

Jennifer Lope naye alikuwemo katika uwanja huo kuushuhudia mchezo huo.

Pia mchezaji wa Clevand Cavaliers Le Bron James alikuwepo, bondia David Haye alikuwepo na mtayrishaji wa muziki na pia mtangazaji Nick Cannon alikuwa mmoja kati ya mastaa wengi waliohudhuria.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata