MAMLAKA YA MAJI KAHAMA YAWANASA WATU 10 WANAOHUJUMU MIUNDO MBINU YA MAJI ENEO LA COOL BREEZE.

 AFISA MAHUSIANO WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KAHAMA JOHN MKAMA AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WATU WALIOKAMATWA WAKITUMIA MAJI YALIYOTOKANA NA UHARIBIFU WA MIUNDO MBINU YA MAJI KWA KUKATA BOMBA.KAHAMA
Watu  kumi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani kahama kwa tuhuma za wizi wa maji katika eneo la COOL BREEZ mjini humo, huku jeshi hilo likiendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine waliokimbia.

Akiongea na Kahama Fm, Afisa mahusiano wa MAMLAKA ya maji  Safi na usafi wa Mazingira mjini Kahama (KUWASA), JOHN MKAMA amesema wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

MKAMA amesema baada ya kuweka mtego walifanikiwa kupata orodha ya watu wote wanaochota maji katika eneo hilo, na kuongeza kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakichota maji kwa njia isiyo halali baada ya kupasua bomba.

Wakiongea katika eneo la Tukio baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hilo wamekiri kutumia maji hayo ambayo hawajui yanakotokea kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa kwa sababu waliona yanamwagika ovyo.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa Tukio hilo huku mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Kahama (KUWASA) ikitoa Onyo kwa wananchi kuacha kuhujumu miundo mbinu ya maji na watoe taarifa pindi wanapoona uharibifu.

MATUKIO KATIKA PICHA:


MAAFISA WA MAMLAKA YA MAJI WAKIWA ENEO LA TUKIO AMBAPO BOMBA LILILOKATWA LINATIRIRISHA MAJI YAKE .


 MOJA YA OFISI AMBAYO INATUMIA MAJI YATOKANAYO NA UHARIBIFU WA BOMBA HILO.

  AFISA MAHUSIANO WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KAHAMA JOHN MKAMA AKIJARIBU KUFUNGULIA MAJI KATIKA MOJA YA BOMBA LILILOKUWA KARIBU NA ENEO LA TUKIO.

  AFISA MAHUSIANO WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KAHAMA JOHN MKAMA AKIWA NA AFISA WA POLISI WALIPOFIKA KATIKA MOJA YA KIJIWE CHA KAHAMA AMBACHO KINASADIKIWA KUTUMIA MAJI KWA NJIA YA UHARIBIFU WA MIUNDO MBINU.


MAONGEZI YAKIENDELEA KATIKA KIJIWE CHA KAHAWA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata