MAMLAKA YA MAJI KAHAMA (KUWASA) YAANZA UJENZI WA MABWAWA YA MAJI TAKA,BODI YATOA ONYO KWA WANANCHI WANAOTIRIRISHA KINYESI.

 
 MENEJA UFUNDI WA MAMLAKA YA MAJI KAHAMA  Eng: LUCHANGANYA PAUL AKITOA MAELEKEZO NAMNA MABWAWA YA MAJI TAKA YATAKAVYOFANYA KAZI.

KAHAMA
MAMLAKA ya maji safi na usafi wa Mazingira wilaya Kahama mkoani Shinyanga (KUWASA) imeanza ujenzi wa mabwawa ya maji taka ili kukabiliana na umwagaji ovyo wa maji hayo katika halmashauri ya mji wa Kahama.

Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti mpya wa bodi ya mamlaka hiyo Meja Mstaafu Bahati Matala katika ziara ya kukagua mabwawa hayo na miundo mbinu ya maji taka katika eneo la Busoka wilayani humo.

Matala amesema mamlaka hiyo imeanza ujenzi wa mabwawa matano ya maji taka yenye uwezo wa kukusanya maji mengi na kutoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kutiririsha maji taka kuacha kufanya hivyo na badala yake watumie mabwawa hayo kumwaga maji taka.

Sambamba na hayo Meja Matala amewataka wafanyabiashara wanaosomba maji taka kuangalia upya bei zao za huduma huku akitoa wito kwa viongozi wa kata ya Busoka kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi karibu na mabwawa hayo kutosogea karibu na mabwawa kutokna na sababu za kiusalama.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Kahama,Injiania Joel Lugemarila amesema kuwa Mradi huo utagharimu Shilingi Milioni 450 na utaanza kufanya kazi ndani ya miezi mitatu.

Kwa mujibu wa Taarifa za Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira wilayani Kahama (KUWASA) halmashauri ya mji wa Kahama inazalisha mita za ujazo elfu sita za maji taka kwa siku.


 MATUKIO KATIKA PICHA:
 MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KAHAMA (KUWASA) MEJA MSTAAFU BAHATI MATALA KUSHOTO AKIWA NA MENEJA UFUNDI WA MAMLAKA HIYO Eng: LUCHANGANYA PAUL KATIKAKATI NA KULIA NI MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA HIYO Eng: JOEL LUGEMARILA WAKIKAGUA MRADI HUO KATIKA ENEO LA BUSOKA.

 MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA MAJI PAMOJA NA WAJUMBE WA BODI HIYO NA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA HIYO WAKIKAGUA UJENZI WA MABWAWA YA MAJI TAKA.
 
 HILI NI MOJA YA BWAWA LA MAJI TAKA LILILOCHIMBWA KATIKA ENEO HILO LA BUSOKA.
 WAJUMBE WA BODI NA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI KAHAMA (KUWASA) WAKIKAGUA SEHEMU AMBAYO ILIKUWA INATUMIKA KUMWAGA MAJI TAKA KIPINDI CHA NYUMA.

GARI LA MAJI TAKA LILILOKUTWA ENEO LA BUSOKA LIKIMWAGA MAJI KATIKA ENEO LA ZAMANI 

MENEJA UFUNDI WA MAMLAKA HIYO Eng: LUCHANGANYA PAUL AKIMPA MAELEZO MWENYEKITI WA BODI YA (KUWASA) MEJA MSTAAFU BAHATI MATALA JINSI MABWAWA HAYO YATAKAVYOKUWA YANAKUSANYA MAJI TAKA.

MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MEJA MSTAAFU BAHATI MATALA AKIKAGUA VIPULI VYA MAMLAKA KATIKA ENEO LA LUGELA AMBAPO KUNA OFISI ZA KUHIFADHIA VIFAA VYA MAMLAKA.


 MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA (KUWASA) JOEL RUGEMARILA AKIMPA MAELEKEZO MWENYEKITI WA BODI KUHUSU MABOMBA YANAVYOHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA MAMLAKA HIYO.

 MENEJA UFUNDI WA MAMLAKA HIYO Eng: LUCHANGANYA PAUL ALIYENYOSHA MKONO AKIMPA MAELEKEZO MWENYEKITI WA BODI NAMNA MAJI YANAVYOTIBIWA KATIKA TANKI KUBWA LA SHUNU NYAHANGA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata