MAJAMBAZI WAVAMIA OFISI ZA DRFA NA KUTAKA SHILINGI MILIONI 150

Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia kwenye ofisi za Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwapora baadhi ya wafanyakazi akiwemo katibu mkuu wa chama hicho, Kanuti Daudi.

Watu hao walivamia ofisi za DRFA leo asubuhi na kufanya uboraji huo huku wakiagiza kupewa Sh milioni 150 zilizokuwa ndani ya ofisi za DRFA.

Katibu huyo amesema, kabla ya kufika, wenzake walionyeshwa silaha kama alivyoelezwa lakini yeye hakuiona.

"Wenzangu wanasema awali walionyesha silaha, mimi sikuiona baada ya kufika ila niliona mmoja akiwa na pingu."

Kanuti amesema baada ya kufika walimtaka kuingia kupanda juu, huko alikuta wafanyakazi wenzake wakiwa wamefungwa.
“Kufika juu nikawakuta wenzangu wakiwa wamefungwa. Nikajumuishwa na kutakiwa kutoa fedha Sh milioni 150 jambo ambalo lilinishangaza, nikawaambia ntazitoa wapi.

“Wakaanza kunisachi na kuchukua ufunguo uliokuwa mfukoni mwangu pamoja na fedha kama Sh lakini mbili hivi. Tayari walikuwa wamewapokonya fedha baadhi ya wafanyakazi wenzangu,” alisema.

“Baada ya kuona hatuna kitu walichokuwa wanakitaka, walifanya uporaji huo wa fedha kwetu pamoja na vifaa kama laptop halafu wakaondoka zao.
“Wana usalama walikuja baadaye sana, maana jamaa walikuwa wameishaondoka na wasamalia wema walikuwa tayari wametufungua.”

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata