MADIWANI USHETU WACHARUKA KUHUSU TAARIFA ZA FEDHA.Madiwani wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wameitaka idara ya fedha na Mipango kuwa makini na uandaaji wa taarifa za fedha ili  kuondoa mkanganyiko unaowafanya madiwani kushindwa kuelewa matumizi halali na salio la fedha lililopo.

Akitoa hoja mara baada ya  kuwasilishwa kwa mapato na matumizi ya mwaka ulioishia juni 30,  Diwani wa kata ya  Nyankende DOA MAKINGI amesema matumizi ya fedha na salio havilingani kwenye taarifa ya bakI na ile ya matumizi.

Amesema kutotolewa kwa taarifa sahihi kunaweza kukasababisha madiwani kushindwa kuelewa kwani baadhi ya fedha zinaonekana kutumika, huku eneo jingine likiwa linaonyesha kuwa bado kuna salio.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu MICHAEL  MATOMOLA amekiri kuwa kuna mkanganyiko kwenye hesabu zilizowasilishwa kwenye baraza hilo, huku akisema kuwa hali hiyo imesababishwa na Mkurugenzi aliyeondoka.

Katika kikao hicho cha baraza la Madiwani, Madiwani hao wamemchagua diwani wa Kata ya Igwamanoni GAGI LALA GAGI kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye ametetea kiti chache, pamoja na viongozi wa Kamati mbalimbali za halmashauri hiyo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata