MACHIEF ORIGIBAL WAPIGA MARUFUKU WANASIASA KUSIMIKWA KUWA MACHIFU.


UMOJA wa Machifu (UMT) umesema haukubaliani na utamaduni unaotaka kujengeka na kuota mizizi kwa baadhi ya makabila kusimika viongozi wa kisiasa kuwa sehemu ya machifu.

Msimamo huo umetolewa baada ya kikao cha UMT kilichokaa wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Pamoja na mambo mengine, UMT imeonyesha masikitiko yake kwa wanasiasa kukabidhiwa zana za jadi bila kufuata taratibu za upatikanaji wa uongozi huo ndani ya jamii husika.

Chifu Isaac Meijo Kisongo ambaye ni Legwanani Mkuu wa Wamasai na Chifu Mpandula Zelandihu wa Kalunde Tabora, walieleza kutokubaliana na utaratibu huo unaoendelea kufanywa na baadhi ya makabila hapa nchini.

“Utaratubu wa kuwapa viongozi wa kisiasa heshima hiyo ya machifu kwa sababu tu ya kutekeleza shughuli za maendeleo wanazozifanya katika jamii ni kinyume kabisa na taratibu na tamaduni za upatikanaji wa machifu katika nchi yetu,”alisema Zelandihu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata