KAMANDA MPYA DAR AWAAMBIA WAHALIFU WATAFUTE PAKWENDA

Kamanda Mpya wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina Lazaro Benedict Mambosasa amewapa salamu watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu Jijini humo.
Akizungumza kwa mara ya kwanza na Waandishi wa habari katika makao makuu ya kanda ya jeshi hilo, Kamanda Mambosasa ametamka kuwa yeye yupo kikazi zaidi na hivyo wahalifu watafute mikoa mingine ya kukimbilia na sio Dar es salaam.
Hata hivyo Mambosasa ameeleza kuwa katika kipindi chake atahakikisha Polisi wake wanafanya kazi kwa uweledi mkubwa ili kuepuka uonevu kwa Wananchi.
Aidha Mambosasa amemaliza kwa kusema kuwa yote hayo yatafanikiwa endapo wananchi watashirikiana na Jeshi la Polisi ili kupafanya Dar es salaam kuwa sehemu ya amani na utulivu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata