APONZWA NA U-JIKE DUME PWANIJeshi la polisi mkoani Pwani linamshikilia kijana mmoja wa kiume (17) mkazi wa Mbagala Dar es Salaam  aliyejifanya mwanamke kwa kuvalia mavazi ya kike kwa lengo linalodaiwa kuwa ni kutaka kufanya uhalifu.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 3 asubuhi huko maeneo ya picha ya ndege barabara ya kwenda magereza wilaya ya Kibaha  mkoa wa Pwani ambapo mtuhumiwa mbali ya kuvaa mavazi ya kike pia alikuwa ameficha uso wake kwa nikabu.

Kamanda wa Polisi alisema kijana huyo alikamatwa na polisi akiwa amepandishwa kwenye bodaboda baada ya wananchi kutoa  taarifa  za siri za kumtilia mashaka mtu huyo.

Shana amedai kwa sasa polisi bado wanafanya mahojiano naye ili kujua lengo lake nini na kubaini mtandao wake anaoshirikiana nao katika kufanya uhalifu.

Wakati huo huo Kamanda Shana amewaonya wananchi mkoani Pwani kuacha kujichukulia sheria mkononi pale wanapowakamata wahalifu badala yake wawafikishe kwenye vyombo vya dola ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Shana alisema hayo baada ya mtu mmoja mkazi wa Mlandizi Abdala Chakame (25) kushambuliwa na wananchi wenye hasira waliokusanyika kituo cha dala dala kongowe baada ya kubaini mtu huyo ni mwizi. Mtu huyo alifariki mara baada ya kufikishwa katika hosptali ya Tumbi baada ya kujeruhiwa vibaya ambapo kabla ya kukutwa na mauti mtu huyo alikiri kuwa alikuwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata