WODI YA WANAWAKE KAHAMA YATIA AIBU,MLANGO UMEHARIBIKA WAGONJWA WANALALA MLANGO WAZI.Halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kukarabati milango na madirisha katika wodi za hospitali ya mji huo ili kuwaepusha wagonjwa waliolazwa kupata magonjwa mengine ikiwemo malaria.

Wakiongea na Kijukuu Blog, MHINA MDASHI na  JOASHI OMOLO ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali hiyo, wamesema kutotengenezwa kwa milango katika wodi za wagonjwa inaonyesha kuwa watendaji hawawajibiki katika nafasi zao.

 
 HIVI NDIVYO HALI ILIVYO YA MLANGO HUO.

Wametolea mfano wodi ya wanawake namba 4 ambayo wamesema milango yake imevujika, hivyo kuwalazimu wagonjwa kulala milango wazi, hali ambayo wanaweza kuungua magonjwa mengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama ABEL SHIJA amesikitishwa na hali hiyo na Kumuagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha milango hiyo inatengenezwa kwani ni aibu kwa halmashauri na inaweza kusababisha magonjwa mengine kwa wagonjwa.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata