WAZIRI MKUU AAGIZA KUKAMATWA KWA VIONGOZI 12 WA JIJI LA MBEYA KWA KUSABAISHA HASARA YA BILIONI 63

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iwakamate watendaji 12 wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakiwamo aliyekuwa mstahiki meya Athanas Kapuga.

Amesema pia wakamatwe, wakurugenzi watatu, kaimu mkurugenzi, wahasibu wawili na wajumbe wa bodi wanne kwa kuisababishia hasara jiji hilo kiasi cha Sh63 bilioni katika ujenzi wa Soko la Mwanjelwa.

Amewataka makamanda wa Takukuru kuanzia leo wawakamate watuhumiwa hao na kwamba anatuma timu kutoka ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kuandaa mashtaka hayo ambapo itatua Mbeya  Jumatano.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata