WATUMISHI KIBAHA VIJIJINI WANAOISHI NJE YA MAENEO YA KAZI WAONYWA

Na Omary Mngindo, Mlandizi

WATUMISHI katika Halmashauri ya Kibaha vijijini Mkoa wa Pwani yenye vijiji zaidi ya 35 na Vitongoji wametakiwa kuishi katika maeeo yao ya kazi badala ya hivi sasa waliowengi kukaa Mlandizi.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mansour Kisebengo alitoa onyo hilo wakati anafunga kikao cha Baraza la Madiwani la robo ya mwisho ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 ambalo limejadili taarifa za Kata 14 zenye vijiji 33 na Vitongoji 104 ambapo alisema kumekuwepo na baadhi ya watendani ngazi za Kata na vijiji pamoja na watumishi wengine kuishi Mlandizi huku wakiacha vituo vyao vya kazi vikikosa watumishi hao.

Alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya maofisa watendaji na watumishi wengine kuishi Mlandiza huku wakiacha maeneo yao ya kazi jambo linalosababisha kero kwa wananchi wanapopatwa na matatizo yanayohitaji utatuzi wa wahusika hao wakati wao hawapo huku akiwataka wajirekebishe mapema kwani si jambo zuri kufukuzana kazi.

"Pia niwaombe viongozi ngazi za vijijini tuwe wabunifu wa katika kuondoka na na baadhi ya changamoto, mfano sisi Kwala tumeweza kutatua baadhi ya kero za wananchi wetu wenyewe pasipokuisubiri halmashauri, tumepekea huduma kwenye shule na hiyo imetokana na kuona uwezo mdogo ilionao halmashauri yetu, tuwe wabunifu katika masuala ya kimaendeleo kwenye maeneo yetu," alisema Mwenyekiti huyo.

Wakichangia mada katika kikao hicho madiwani Josephina Gunda Viti Maalumu Kata ya Kwala,  Mkali Kanusu Kata ya Dutumi wa CCM na Issa Mkali wa Magindu kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA walichuana vikali katika mada ya upekekwaji wa huduma ya maji katika shule ya sekondari ya Kata ambapo Issa aliiomba halmashauri isaidie upatikanaji wa kiasi cha sh. Laki 9 kufanikisha zoezi hilo.

Ombi hilo liliwaibua madiwani Gunda na Kanusu ambao walimtaka diwani huyo kutumia mamlaka hake kushawishi wadau waliopo kwenye maeneo yake katika utafuta kiasi hicho walichokieleza ni kidogo ukulinganisha na wadau waliopo eneo hilo huku wakisema kama atadhindwa kufanya hivyo atakiwa amedhindwa nafasi hiyo, aachie ngazi.

"Mheshimiwa Isa ni diwani wa Kata ya Magindu, haiwezekani ndani ya Kata yako mkashindwa kutafuta kiasi cha sh. Laki 9 kwa ajili ya kufikisha maji katika shule mpaka muitegemee halmashauri, inaonekana hutoshi ni bora ukakaa pembeni," alisema Kanusu.

Akijibu hilo Issa aliema kuwa shule hiyo inatoa huduma kwa wananchi wa halmashauri nzima Kibaha yenye Kata 14 na vijiji 35 kwa maana ya wanaoishi Magindu na maeneo mengine hivyo suala hilo linapashwa kubebwa na halmashauri pamoja na wadau wengine mbalimbali wa kimaendeleo.

"Ile shule inatoa huduma kwa wakazi wote wa halmashauri ya Kibaha Vijijini na si kwa watu wa Magindu pekee kwani wanaosoma pale wanatoka Mlandizi na maeneo mengine hivyo tukitaka kufanya shughuli za imaendeleo tuangalie uhalisia na si vinginevyo," alisema Issa.

MWISHO.

Picha ya tatu Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Mansour Kisebengo akizungumza wakati anafunga kikao cha Madiwani wa halmashauri hiyo. Picha na Omary Mngindo


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata