WANANCHI WA KAKEBE KAHAMA WAMKATAA MWENYEKITI WA KIJIJI,KISA HAWASHIRIKISHI KATIKA MASWALA YA MAENDELEO.Wananchi na wajumbe wa kamati ya serikali ya kijiji cha KAKEBE kata ya NYANDENDWA Halmashauri ya mji wa Kahama wamemkataa  mwenyekiti wao JUMA JOHN kwa madai ya kutowashirikisha katika  shughuli za  maendeleo.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliyofanyika jana kijijini hapo wananchi hao wamesema tangu mwenyekiti huyo aingie madarakani hajawahi kuwashirikisha kwa jambo lolote la maendeleo bali huchukua maamuzi binafsi.

Wamesema mpaka sasa wajumbe wa kamati ya serikali ya kijiji wamejiondoa kwenye kamati hiyo na hawataki kushirikiana naye kutokana na  kuwateua wajumbe anaowataka yeye.

Kwa upande wake mwenyekiti huyo JUMA JOHN amesema tatizo ni yeye kufanya maamuzi ya kuweka wajumbe katika kamati ya serikali ya kijiji, jambo ambalo kimsingi liko kisheria.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata