TUNDU LISSU AZUNGUMZIA SAKATA LA MADIWANI WA CHADEMA KUHAMIA CCM........PIA KAZITAJA SABABU ZA CHADEMA KUINGILIA MGOGORO WA CUF

Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Tundu Lissu amesema Ukawa unatangaza vita na CUF ya Profesa Ibrahim Lipumba kama walivyo vitani na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lissu ameyasema hayo jana wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni, Jijini Dar es salaam.

Alisema kwa kuwa chama hicho ni miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA, watahakikisha wanaingia vitani kumong’oa Prof. Ibrahim Lipumba aliyedai kuwa ni msaliti

“Profesa Lipumba ametusaliti kwa kuwa yeye ndiye aliyempitisha Lowassa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Ukawa. CUF ya Lipumba ilitusaliti kama Yuda Iskarioti alivyomsaliti Yesu Kristo,” alisema Lissu.

Mgogoro wa CHADEMA na CUF ya Lipumba ulianza baada ya kiongozi huyo kuandika barua ya kujiuzulu Uenyekiti wa chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015 na baadaye kutaka kurejea katika nafasi yake hali iliyosababisha mpasuko ndani ya Ukawa pamoja na CUF kwa ujumla.
Akizungumzia kuhusu kitendo cha baadhi ya madiwani na wenyeviti wa chama hicho kuhamia CCM kutokana na hali ya kuridhishwa na uchapakazi wa Rais John Magufuli, Tundu Lissu aliwavaa viongozi hao na kuwatuhumu kuwa   wamekiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1997 na kwamba wamekiuka viapo vya maadili kwa sababu kuhama kwao kumesukumwa na rushwa.

Alidai kwamba, mmoja wa viongozi hao ambaye hakumtaja jina, wiki moja baada ya kuhamia CCM aliteuliwa kuwa Mchumi wa Halmashauri ya Arumeru, jambo ambalo amelifananisha na kula rushwa.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata