RC MTWARA ATOA SIKU 7 KUKAMATWA WASICHANA WALIOPATA MIMBA


Mkuu wa mkoa wa mtwara Bibi. Halima Dendego ametoa siku 7 kukamatwa wasichana waliopata mimba Mtwara.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mtwara Bibi. Halima Omar Dendego alitoa uamuzi huo kwenye mkutano wa hadhara wilaya ya newala 
Mapema, alipofika kijiji cha mikumbi na kupokea taarifa kuwa kati ya januari hadi july mwaka huu, wanafunzi 8 wa shule ya sekondari mikumbi wamepata mimba, mkuu huyo wa mkoa ametoa siku 7 kwa polis kuwakamata wasichana waliopata mimba na wanaume waliowapa mimba, na kuwafungulia kesi; na apewe taarifa juu ya utekelezaji wa agizo hilo mara moja.
Kwenye ziara hiyo ya siku 4 wilaya ya newala ya kuhamasisha maendeleo na kusikiliza kero za wananchi, mkuu huyo wa mkoa wa mtwara bibi halima omari dendego wamezuia mishahara ya maafisa watendaji kata 2 na afisa mtendaji wa kijiji 1 kwa kushindwa kuhamasisha wananchi kufyetua matofali ya kuchoma milioni moja kwa kila kijiji au matofali ya saruji laki 3 maarufu benki ya matofali, tangu alipoagiza mwezi julya mwaka jana, ambayo yangesaidia kuondoa kero ya ujenzi wa nyumba za waalimu na ujenzi wa zahanati.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata