PRECISIONAIR KUANZA KUTOA HUDUMA YA USAFIRI WA ANGA WILAYANI KAHAMA JUMAPILI HII.


SHIRIKA la ndege la PrecisionAir linaanza kutoa huduma ya usafiri wa anga wilayani kahama mkoani Shinyanga kuanzia jumapili hii July 16.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari,Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhil Nkulu amesema kuwa ndege hiyo itatua saa 16:30 jioni katika uwanja wa ndege wa Buzwagi ambao kwa sasa umepanuliwa.

Nkulu ameongeza kuwa ngege hiyo itakuwa ikifanya safari zake kutoka Kahama…kwenda Dar es salaam na Tabora.

Ameongeza kuwa hiyo ni fursa kwa wakazi wa Kahama na maeneo jirani kutumia usafiri huo ambao utarahisisha safari zao za Tabora na Dar es salaam.

Akiongelea kuhusu ubora wa Kiwanja cha Ndege Nkulu amesema uwanja huo kwa sasa Umepanuliwa na kukarabatiwa tofauti na ilivyokuwa awali.

 SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata