POLISI BUKOMBE,WAMUOMBA MBUNGE BITEKO AWASAIDIE KUTATUA KERO YA USAFIRI.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisaini kwenye kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Kituo cha Polisi Runzewe.
 
 
Polisi wa Kituo cha  Runzewe  Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwatatulia changamoto ya usafiri kwenye Kituo hicho cha Polisi Runzewe. 

Wakati akizungumza Mkuu wa Kitu hicho Insp. Richard Godbless Mkesi amesema hali ya usalama kwa maeneo hayo iko shwari na kumbainishia changamoto ya ukosefu wa usafiri kituoni hapo kutokana na uchakavu wa magari na kukosa matengenezo ya magari hayo kunawasababishia hali ya kufanya shuguli zao za kiusalama kwa kuazimaazima usafiri.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko aliwashukuru kwa kazi nzuri ya kuimarisha ulinzi na usalama wa maeneo hayo na kuwaomba polisi hao kuzidi kuwaelimisha wananchi juu ya kutii sheria bila shurti hasa kwenye vyombo vya moto. 

Pia aliahidi kushirikiana na polisi hao pamoja na wananchi wa maeneo hayo na Wilaya nzima kwa ujumla katika kuhakikisha watumiao vyombo vya moto hasa bodaboda wanapatiwa mafunzo ya usalama barabarani ili kupunguza ajali na vifo visivyokuwa vya lazima na hatimae kupoteza nguvu kazi ya taifa.
 
 Mkuu wa Kituo cha Polisi Runzewe hicho Insp. Richard Godbless Mkesi akimweleza Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Picha ya Kituo cha Polisi Runzewe.

Haya ni magari ya Kituo cha Polisi Runzewe
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya askari polisi wa Kituo cha Polisi Runzewe.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya wananchi waliokuwa maeneo ya kituo hicho cha polisi Runzewe.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata