MWANAMKE AUAWA KIBAHA,POLISI WATANGAZA MAPAMBANO DHIDI YA WAHALIFU

Baada ya mkazi wa Mharani kwa Matiasi wilayani Kibaha kukutwa amefariki dunia kwa kuuawa na watu wasiojulikana jana majira ya saa moja usiku, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Jonathan Shana ametangaza mapambano makali ya kuwatia nguvuni wahalifu.
Kamanda Shana amesema kuwa mwili wa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu Omari (31) ulikutwa nje ya nyumba anayoishi mbele kidogo umbali wa mita 40 akiwa anavuja damu nyingi sehemu za usoni na jereha kichwani upande wa kushoto huku muuaji akiwa bado hajafahamika

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata