MGODI WA ACACIA BULYANHULU WALIPA SHILINGI MILIONI 460 YA USHURU WA HUDUMA KWA HALMASHAURI YA MSALALA

Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala. 
############################
 
 KAHAMA

Kuzuiliwa kwa usafirishaji wa mchanga wa madini (MAKINIKIA)  nje ya nchi, kumesababisha kampuni ya Acacia kupunguza malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Msalala wilayani KAHAMA kwa kipindi cha January – June 2017.

Hayo yamebainishwa leo na mkurugenzi wa halmashauri ya MSALALA SIMON BEREGE wakati akipokea hundi ya ushuru wa huduma (SERVICE LEVY) ya zaidi ya shilingi milioni 460.7 iliyokabidhiwa kwa halmashauri na mgodi wa acacia Bulyanhulu.

BEREGE amesema wamepokea mapato hayo kwa upungufu wa zaidi ya shilingi milioni 300 iikilinganishwa na mwaka jana ambapo ilikuwa zaidi ya shilingi milioni 700, na kwamba bado wanasubiri muafaka wa mazungumzo kati ya serikali na wawekezaji ili kuboresha ulipwaji wa mapato hayo kama awali.

Naye mkuu wa wilaya ya KAHAMA FADHILI NKURLU amewashukuru acacia kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika  kutoa huduma kwa jamii huku akikiri kupungua kwa mapato hayo.

Awali akikabidhi hundi hiyo MENEJA MKUU WA MGODI huo profesa Graham Crew amesema lengo la mgodi huo ni kuendeleza mahusiano mazuri kati ya mgodi na Halmashauri ya msalala na kuendelea kuwekezaa pamoja katika kusaidia jamii inayozunguka mgodi huo.

 MATUKIO KATIKA PICHA:
Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala. 

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo Jumatano Julai 26,2017 katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 iliyotolewa na Mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (kulia) akishikana mkono na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew wakati wa zoezi la kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati akimkabidhi hundi hiyo Kaimu Mweka Hazina wa halmashauri hiyo Saleh Bugege (kushoto). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah Ezra Terry.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata