MAKINIKIA YA BUZWAGI YASABABISHA MALIPO YA USHURU WA HUDUMA KUWA PUNGUFU.

Halmashauri ya mji wa Kahama leo imepokea malipo ya Ushuru wa Huduma shilingi milioni 455 kutoka mgodi wa ACACIA-Buzwagi kwa kipindi cha Januari hadi Juni Mwaka 2017 huku kiwango kikipungua kwa zaidi ya nusu ikilinganishwa na  miaka iliyopita. 

Kufuatia kushuka kwa malipo hayo, Mkuu wa wilaya ya Kahama FADHIL NKULU amewaambia waandishi wa Habari kwamba, kiwango hicho kimepungua kufutia kusimama kwa biashara ya makinikia ambapo yatakapouzwa sehemu iliyobaki italipwa tena kwa halmashauri hiyo.

NKULU amefafanua kuwa kutokana na maelezo ya meneja Mkuu wa Mgodi huo STEWART HAMILTON, jumla ya makontena 900 ya makinikia yanasubiri kuuzwa mgodini humo na kwamba asilimia 0.3 ya mapato yatakayopatikana italipwa tena kwa halmashauri hiyo...

Amesema, ofisi yake pia inatambua kuwepo kwa malimbikizo ya madai ya iliyokuwa halmashauri ya wilaya ya Kahama kwa mgodi huo, jumla ya shilingi bilioni 9, suala ambalo liko serikali kuu, ambayo imeliweka katika majalianao na ACACIA yanayoendelea ...

NKULU amesisitiza pesa hiyo kuunganishwa na milioni 800 zilizolipwa mwaka jana kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama, huku akiwahimiza watu wa TBA kuharakisha mchakato wa ujenzi huo kwa kuwa pesa zipo..

Usafirishaji wa Makinikia kwenda nje ya nchi umesitishwa na Serikali kufuatia amri ya rais Dakta JOHN MAGUFULI alipopokea taarifa ya kamati mbili zilizokuwa zikichunguza biashara ya makinikia, hali iliyosababisha kuanza kwa mazungumzo mapya kati ya Serikali na ACACIA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata