MAJALIWA: UFUTA KUNUNULIWA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI


SERIKALI imesema kuanzia msimu ujao zao la ufuta litanunuliwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, ili  wakulima wa zao hilo waweze kupata bei nzuri. Hayo yamesemwa leo na waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, aliposimama kuwasalimu wananchi katika kijiji cha Kibutuka wilaya ya Liwale.

Ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku nne katika mkoa huu wa Lindi. Waziri mkuu Majaliwa alisema, awali viongozi wa mikoa ya Lindi na Mtwara walikusudia kuliingiza zao hilo kwenye mfumo huo. Hata hivyo ilishindikana.

 Kwasababu mpango huo haukuyashirikisha makundi mengine. Ikiwamo wananchi. Pia Majaliwa amewataka wananchi kuunga mkono mpango huo pindi utakapoanza. Huku alionya kuwa serikali haikubali na haitakubali kuona walanguzi wananunua zao hilo. ikiwa ni kinyume cha sheria.

Alisema hivi sasa zao hilo linanunuliwa kwa bei ndogo kutokana na kukosekana mfumo rasimi wa ununuzi na uuzaji wa zao hilo. Hali inayotoa nafasi kwa walanguzi kuwarubuni na kuwapunja wakulima. Akizungumzia changamoto ya barabara ya Nachingwea hadi Liwale, Waziri Majaliwa alisema barabara hiyo ni miongoni mwa barabara zilizo kwenye mpango wa kufanyiwa matengenezo.

 Akibainisha kwamba hatua ya kwanza itakuwa ni kuifanyia upembuzi yakinifu. Hata hivyo aliweka wazi kuwa  mwaka huu wa fedha, barabara ya Masasi, Nachingwea hadi Nanganga itaanza kutengenezwa kwa kiwango cha lami. Ambapo pia barabara ya Nachingwea, Ruangwa hadi Kiranjeranje ipo kwenye mpango.

Ni kutokana na umuhimu wake. Ikiwamo kupunguza umbali wa safari na usafirishaji kutoka Songea hadi Dar - eS-salaam. Aliongeza kusema kuwa barabara ya Liwale hadi Nanguruku hajasahauliwa, bali inakumbukwa na itatengenezwa pindi uwezo wa kifedha usiruhusu. Majaliwa ameanza ziara yake katika wilaya ya Liwale katika ziara yake ya siku nne katika mkoa huu wa Lindi. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi baada ya kumaliza katika wilaya ya Liwale atakwenda wilaya ni Ruangwa. Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo katika wilaya ya Lindi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata