KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWATAKA WATANZIA KUSIMAMIA MALIASILI NA KUPAMBANA NA WEZI WA MADINI KAMA ANAVYOFANYA RAIS MAGUFULI.

Watanzania wametakiwa kushiriki katika kusimamia maliasili zilizopo katika maeneo yao na kupambana na wezi hasa wa Madini kama rais  Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI alivyoanzisha mapambano hayo.

Wito huo umetolewa leo katika kata ya CHELA Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama na Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, AMOUR HAMAD AMOUR wakati akitoa  ujumbe wa Mwenge wa Uhuru, baada ya Mwenge huo kuwasili katika Halmashauri hiyo.

AMOUR amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwa kamati mbalimbali zinazofika kwa ajili ya kukagua mali asili za nchi ili kuhakikisha zinawanufaisha wananchi wanaozizunguka.

Amesema anasikitika kuona wananchi wa Halmashauri ya Msalala wakiishi katika hali ya umasikini, licha ya kuwa na migodi ya Dhahabu katika eneo hilo.

Katika halmashauri ya Msalala, Mwenge huo  wa Uhuru tayari umezindua Soko na Ghala la mazao katika kijiji cha Bulige, mradi wa maji safi yanayotoka ziwa Victoria katika kijiji cha Igombe na kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Ngaya hadi Busangi yenye urefu wa kilomita 8.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata