JIJI LA DAR ES SALAAM KUFUNGWA KAMERA KILA KONA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amefanya mkutano wa majadiliano na wadau wa Usalama kujadili mfumo wa teknolojia ya ufuatiliaji wa Vyombo vya usafiri na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kutumia Camera za kisasa.

Mfumo huo ujulikanao kama Tanzania Tracking Technology of Security Monitoring System umejumuisha wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni ya ulinzi ya TAMOBA Ltd,TTCL na VETA ambapo utakuwa na uwezo wa kutambua Gari,namba za Gari, sehemu Gari ilipo,jina la Dereva pamoja na uwezo wa kuizima Gari iliyoibiwa na kutoa taarifa za sehemu Dereva alipokiuka sheria za barabarani.
Mheshimiwa Makonda amebaini mfumo huo unaweza kuleta manufaa katika Nyanja zaidi ya 17 ikiwemo kuzuia makosa ya Barabarani, wizi wa magari,ubovu wa magari, ujambazi, leseni,usalama kwa wageni,Usalama wa raia, kudhibiti bandari bubu pamoja na uharibifu wa barabara utokanao na magari yanayobeba mizigo mkubwa kuliko uwezo wa Barabara.

Aidha Makonda ametoa siku kumi kwa wadau mbalimbali ikiwemo wanasheria, Jeshi la Polisi, VETA, Kampuni ya TTCL, Chuo cha DIT, Chuo kikuu,TRA na Kampuni ya ulinzi ya TAMOBA kuunda jopo litakalopitia mfumo huo na kuja na majibu ya namna ya kutengeneza mfumo kulingana na mazingira na jiografia ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Mimi Story sizipendi, tumepiga story sana,nataka kuona Mfumo wa Camera za CCTV zinafungwa, nakumbuka Rais Mstaafu alishaagiza huu mfumo kuanza lakini hadi leo hakuna lolote, wapo walioenda Nchi mbalimbali ikiwemo China kujifunza huu mfumo lakini hadi leo sijaona lolote, sasa mimi siendi Nchi yoyote, nipo hapahapa Dar es salaam na nitahakikisha Camera zinafungwa”_Alisema Makonda.
RC Makonda ameipa siku 10 kamati atakayoiteua kutoa majibu na utaratibu mzuri wa kisheria kwa namna mfumo huo utakavyo fanya kazi na Idara ya Sumatra, TRA na Polisi

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata