HII NDIO RATIBA YA MAZISHI YA MTANGAZAJI ‘BIKIRA WA KISUKUMA’ KESHO


Aliyekuwa mtangazaji EFM. Marehemu, Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’.
 Meneja Mkuu wa Radio Efm na TV-E,  Dennis Ssebo, ametoa ratiba ya mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wao Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma‘, amesema kesho saa tatu asubuhi mwili wa marehemu utachukuliwa kutoka nyumbani kwa baba yake Changanyikeni, jijini Dar es Salaam, kuelekea viwanja vya Leaders Club ambako utapokelewa na wazazi wake, viongozi wa serikalina wadau mbalimbali.

Baada ya hapo patafanyika misa ya kumuombea marehemu na kufuatiwa na salamu za rambirambi ambapo kuanzia saa 6 hadi saa 8 utakuwa ni muda wa kumuaga marehemu ambapo safari ya kuelekea makaburini kwa ajili ya mazishi itaanza.

Mazishi yatafanyika kuanzisha saa 9 alasiri katika makaburi ya Kinondoni, ambapo wananchi wa Dar es Salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi kumzika ndugu yao Seth Katende.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa; jina lake lihimidiwe!

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata