HARMONIZER AIPANIA KAHAMA USIKU WA LEO,ASEMA NI MARA YAKE YA KWANZA KUJA KAHAMA HIVYO ATAKACHOFANYA HAKIJAWAHI KUTOKEA.

 MSANI HARMONIZE AKIWA KATIKA MAHOJIANO KATIKA KIPINDI CHA LADHA 360 CHA KAHAMA FM.


KAHAMA
 Msanii wa Bongo Fleva kutoka WCB Harmonizer a.k.a Konde Boy amehaidi kufanya Show matata mjini Kahama katika ukumbi wa Kikwetu kwetu Pub.

Akiongea katika kipindi cha Ladha 360 cha Kahama Fm,Harmonizer amesema amejipanga kufanya kufuru katika Show ya leo kwani ni mara yake ya kwanza kufanya Show mjini Kahama hivyo anataka kuwaonyesha wana Kahama uwezo wake wa Kuimba na kutawala jukwaa akiwa na Madancer wake.

Show hiyo ya Harmo Night itafanyika leo (July 21) kuanzia saa mbili usiku katika Ukumbi wa Kikwetu kwetu Pub huku kiingilio kikiwa ni Shilingi elfu 10 tu.

 MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA LADHA 360 CHA KAHAMA FM ALLY TZ AKIFANYA MAHOJIANO NA HARMONIZER

GARI YA TOUR YA HARMONIZER MARA BAADA YA KUTUA KATIKA STUDIO ZA KAHAMA FM

 HARMONIZER a.k.a KONDE BOY AKIWA KATIKA STUDIO TWO ZA KAHAMA FM.

 HAPA KONDE BOY AKIZUNGUMZIA TATOO ZAKE ANAZOCHORA MWILINI,KIKUBWA AMESEMA TATOO YA DIAOMOND ALIYOCHORA NI KUONYESHA NAMNA ANAVYOMKUBALI KWANI AMEMTUOA MBALI KIMZIKI.\

 ALLY TZ WA KAHAMA FM AKISOMA JUMBE ZA WASIKILIZAJI WALIOKUWA WANAULIZA MASWALI YA MOJA KWA MOJA.

 MAHOJIANO YAKIENDELEA NDANI YA STUDIO ZA KAHAMA FM.

 MARA BAADA YA MAHOJIANO HAPA KONDE BOY AKIINGIZA JINGLE NDANI YA PRODUCTION ZA KAHAMA FM 

 KONDE BOY AKIWA NA SEBASTIAN MNAKAYA WA KAHAMA FM MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA BAHARI YA MAPENZI.

 KUTOKA KUSHOTO NI SEBASTIAN MNAKAYA AKIWA NA HARMONIZE NA KULIA NI BAKARI KHALID PRODUCTION MANAGER WA KAHAMA FM.

 HARMONIZER AKIWA NA WILLIAM BUNDALA (KIJUKUU CHA BIBI K) PROGRAM MANAGER WA KAHAMA FM.

 MARA BAADA YA MAHOJIANO KONDE BOY HAPA AKIONDOKA KUTOKA KATIKA OFISI ZA KAHAMA FM 

UMATI WA WATU ULIOFURIKA NJE YA OFISI ZA KAHAMA FM,WAKISALIMIANA NA KONDE BOY MUDA MCHACHE BAADA YA KUMALIZA MAHOJIANO

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata